29 Septemba 2012 - 20:30

Msemaji mkuu wa jamhuri ya Misri amesisitiza kuwa mazungumzo kuhusu kukodisha Kanał ya Sueski kwa Qatar ni kichekesho

Shiirika la Habari la Ahlul Bayt (a.s)-ABNA: Yaasir Ally, msemaji mkuu wa Jamhuri ya Misri amesema: mahusiano ya Misri na Qatar kwa sasa ni mazuri katika kila nyanja, kiuchumi na kisiasa.Ameyazungumza hayo katika mazungumzo na waandishi wa habari  Cairo katika ofisi ya Ikulu ya nchi ya Misri alipokuwa akijibu swali la mmoja kati ya waandishi wa habari aliyeuliza kuwa: Hivi ni kweli Qatar imeacha kuiuzia Misri gesi kwasababu ya kukutaa Misri kuikodisha Qatar Suez Canal ?. alijibu kwa kusema hivyo ni kichekesho si sahihi kuwa nchi kubwa kama Misri kukodisha kitegauchumi chake muhimu na moja kati ya vyanzo vya mapato ya nchi.Naye alimalizia kwa kusema kuwa uhusiano wa Qatar na Misri ni imara mno na hakujatokea tatizo lolote lenye kusababisha kuharibu usiano wetu.